Jumanne 25 Novemba 2025 - 20:33
Maonesho ya Kwanza ya Sanaa ya Kiislamu nchini Korea Kusini Yawashangaza Wahudhuriaji

Hawza/ Jumba la Makumbusho la Taifa la Korea Kusini limeitenga sehemu ya ghorofa ya tatu ya jengo lake kuwa hifadha ya sanaa za Kiislamu, na imepangwa kuwa kuanzia Ijumaa sehemu hii itakuwa wazi kwa umma.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, galari ya sanaa ya Kiislamu iliyopo katika ghorofa ya tatu ya kumbi za kudumu za maonesho ya Jumba la Makumbusho la Taifa la Korea Kusini, inatarajiwa kufunguliwa kwa umma siku ya Ijumaa.

Kutokana na mnasaba wa uzinduzi wa sehemu hii, jumba hilo linakuwa mwenyeji wa maonyesho ya pamoja na Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu mjini Doha, Qatar, yenye anuani isemayo “Sanaa ya Kiislamu: Safari ya Utukufu na Uadilifu, yaliyopangwa kwa ajili ya wageni kutembelea. Maonyesho haya yataendelea kwa muda wa miezi 11 na yanaonesha kazi 83 zilizokopwa Doha.

Jumba la Makumbusho la Taifa la Korea Kusini kwa muda sasa limezindua sehemu ya kuonesha sanaa za maeneo mbalimbali duniani, na tangia wakati huo limekuwa likionesha urithi wa sehemu tofauti tofauti. Hata hivyo, hii ni mara ya kwanza ambapo utamaduni wa Kiislamu unawekwa katika sehemu ya kudumu ya maonyesho haya mbele ya umma.

Maonyesho haya yanachunguza zaidi ya milenia moja ya sanaa ya Kiislamu kuanzia karne ya saba hadi karne ya kumi na tisa, na yanayagawanya kazi hizo katika sehemu kuu tatu: Sanaa za kidini, mabadilishano na uenezaji wa utamaduni wa Kiislamu, pamoja na sanaa ya khatt (kaligrafia ya Kiislamu).

Mojawapo ya mambo mazuri yanayovutia katika maonyesho haya ni kwamba eneo la maonyesho limebuniwa kiusanifu kwa dari iliyo katika umbo la kuba na muundo wa pembenene nane, ili kuwaathiri wageni kana kwamba wanaingia msikitini.

Chanzo: YONHAP NEWS AGENCY

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha